Tuesday, January 8, 2013

NI MARUFUKU!!!(0001)

EXTRACTED FROM FACEBOOK!!!

Ni marufuku kwa mwanafunzi yeyote yule na ninyi wasomi ambao mmetoka shule juzi juzi na mmepata vijikazi ama japo mahali pa kushika kuwadharau ndugu,jamaa,marafiki na watu wanaowazunguka eti tu kwasababu hawajasoma kama ninyi,na kuna watu ni wapumbavu sana,yaani kupata degree tu unaanza kuwadharau mpaka wazazi hali ni wao wamefanya mpaka umefika hapo,unashangaa mtu anajitenga na jamii yake nakujiona wa juu kumbe ujinga tu,basi mikutano ya mtaani haendi,misibani haendi,kufanya kazi ama usafi mtaani au kanisani au kokote kule wanakoitaajika wanajamii wote haendi,shughuli za vijana wenziwe hachangii wala haendi...hivi unadhani kufanya kazi huko mjini na kuvaa tai ndio kunaongeza thamani yako na kuishusha ya kondakta,muuza magazeti au kahawa? Hivi hujui mkopo wote uliokuwa unaupata chuo ni mchango wa kodi wa watu hao unaowadharau kama makondakta?....acha ujinga kijana,kaa chini na watu ujifunze ya watu,mambo mazuri wakati mwingine hupatkana kwa wale unaowadharau!!
NGOJA NIKUPE MFANO HUU WA KWELI.....
....Kuna Prof. mmoja yuko pale mlimani,hujifanya busy,mjuaji,madharau na yuko rafu mpaka dah,
....sasa pia maeneo ya shule yake(kitivo)kuna kichaa mmoja ambaye huwa akizunguka zunguka mara nyingi na kichaa huyo kila mtu humdharau!
....siku moja kuna wanafunzi wenye hasira na yule Prof(na hao ni mmoja ya wajinga ninaowasema) walienda wakatoa upepo kwenye tairi la mbele na kufungua nati wakaondoka nazo ili tu kumkomesha Prof.
......Sasa wakati Prof.anataka kuondoka akakuta dhahama hiyo,basi akabaki kujifyonya pale na akawa amefanya maamuzi ya kutaka kuondoka maana alikuwa ana spare tairi lakini nati hakuna....basi akiwa amekasirika mara akatokea yule kichaa na kumwambia.."Shikamoo Prof! naona wamejaribu kukukomoa hahahah ila bado unaweza kwenda tu,Basi yule Prof.akamtukana kwa kizungu na kumfukuza,ila yule kichaa akasema....sawa ila mimi ningekuwa wewe "ningefungua nati moja moja kwa matairi yote yaliyobaki na kufungia hilo moja kisha ningetafuta nati zingine baadae lakini ningeshafika nyumbani" kisha akaenda zake!!.....Sasa yule Prof.akawaza maneno ya kichaa na kuona yana mantiki na ukweli ndio yaliyomfikisha home kwake!!!
SASA MIMI NAWAAMBIENI NIYI MNAOJIFANYA WASOMI KUPITILIZA MPAKA KUWADHARAU WENGINE,NI MARUFUKU!!!


http://www.facebook.com/chavalapf/posts/10151225935103543?comment_id=24523559&ref=notif&notif_t=comment_mention

No comments:

Post a Comment