Monday, November 4, 2013

"FULLY CHARGED" NDIO THEME YA IBAADA MAALUM YA WANAFUNZI KUANZA MWAKA MPYA WA MASOMO 213/14!!!

 HABARI KAMA ILIVYONUKULIWA TOKA http://vcctcampusministry.blogspot.com/
 
Ile baada maalum ya kuweka wakfu wanafunzi wa vyuo vikuu kwa ajili ya mwaka mpya wa masomo ambayo iliandaliwa na Kanisa la Victory Christian Centre Tabernacle (VCCT) linaloongozwa na Mch. Dr. Huruma Nkone chini ya Idara ya Wanafunzi (Campus Ministry) imekuwa ya aina yake na ya kipekee. wanafunzi toka kila kona ya jiji la Dar es salaam walikusanyika katika kanisa la VCCT lililopo Mbezi A jijini Dar es salaam

Kwaya na vikundi mbali mbali vilikuwepo kumtukuza Mungu katika siku hii. miongoni mwa vikundi vilivyo hudumu ni Mabibo Christian Fellowship Choir toka UDMCF, Kwaya ya CASFETA Dar es salaam, Kwaya toka Chuo cha DIT, Kwaya toka Ardhi University (TAFES Praise team) na Kundi la Glorious Worship Team (GWT) bila kusahau watoto wa nyumba ya VCCT The Rivers of Joy International (RoJI).

Ibada hii ya shangwe iliongozwa na Dr. Huruma Nkone na kuratibiwa na Idara ya wanafunzi (Campus Ministry).

Katika siku hii wanafunzi wa vyuo walipata fursa ya kusikiliza neno toka kwa Mch. Dr. Nkone, na baada ya hapo, Dr. Nkone alifanya maombi maalum kwa ajili ya wanafunzi kwa ajili ya kuwaweka wakfu kwa ajili ya mwaka mpya wa masomo, na baada ya ibada Dr. Nkone alikutana na wanafunzi hao kwenye eneo maalum lililoandaliwa kwa ajili yao na kupata soda pamoja na wanafunzi hao na kisha kuomba baaraka kwa ajili yao.

Tukio la kupiga picha lilifuata ambapo viongozi wa fellowship walipata fursa ya kupiga picha na Mchungaji Dr. Nkone katika red carpet iliyoandaliwa kwa ajili yao.

Angalia matukio yalivyokwenda 


watu waliohudhuria

DR. Nkone akishusha nondo

wanafunzi wakiwekwa wakfu

watu wakimpa Yesu maisha yao

Take note.....Dr. Nkone akiongea na wanafunzi kwa karibu zaidi

The Red Carpet..


Moderator 1st service, CEO wa MANCON EA LTD, Brother Pro

DIT Choir wakimtuza MUngu
watu wakienda sawa
The Bomby, Fredy Msungu na Amani Kapama wakifanya kweli
Ardhi University Tafes Praise team
Campus Ministry team na Dr. Nkone
Kairuki University Pamoja na Mch DR. Nkone
Pokeaaaa kwa Jina la Yesu Kristo

UDMCF Praise team wakiimba

RoJI watoto wa Nyumbani wakiimba