MTOTO NA KANISA
kutana na Victor John mwanafunzi wa chuo kikuu cha Dodoma, mtumishi wa Mungu ambaye anatarajia kuzindua album yake mwishoni mwa wiki hii Jumaamosi ya tarehe 12 mwezi huu wa kwanza ikiwa ni Uzinduzi wa kwanza hapa UDOM kwa mwaka 2013 pale "Social Science Taji Cafeteria" kuanzia saa kumi na mbili jioni hadi saa sita usiku (1800-0000hrs).
Kitu kilichonivutia hasa ni Jina la Album na lengo hasa la kutoa album hiyo. Kama umewahi kufundisha watoto au umewahi kuakaa karibu na watoto, ama unao au unatarajia kuwa na watoto, utamshukuru Mungu kwa ajili ya Victor kwa haya maono aliyompa!
Haya ni maneno yake mwenyewe Victor aliyoniambia pale nilipotaka kujua hasa kuhusu jambo hili
"Jina la album MTOTO NA KANISA (mlee mtoto katika njia impasayo nae hataicha hata atakapokua mzee)
Dhima ya album hii ni kufanya 'restoration' ya nafasi ya mtoto kanisani ili siku za usoni aje kuwa kifaa bora, in 'many cases' leo makanisani unakuta watoto wa waamini ndio wanaosikia kwa maovu kuliko hata watu wengine. Hii inatokana na kukosa malezi bora ya Kimungu. Mfano ni rahisi sana watoto kuambiwa wawapishe wakubwa kwenye viti ili wakubwa wakae na watoto hao wanaishia kupelekwa nje. 'Unknowingly' wanaharibu kizazi kijacho kwa taifa na kanisa pia. 'So in my album' nimeongea umuhimu wa kumlea mtoto katika maadilimya kimungu. 'By the way my parents are priests', nimeona tofauti kati ya kumlea mtoto katika njia inayompasa na njia isiyompasa. Laiti kama nisingelelewa katika njia inipasayo sijui hata kama leo ningekua UDOM. 'This album' inagusa maisha yangu binafsi, na nataka kanisa lifanye 'as the way' nilivyolelewa ili kisiwepo kizazi kitakachohatarisha mustakabali wa kanisa na taifa pia.
Nimefanya kazi na huduma ya watoto na vijana tabora (HUIMA) na natamani kuendelea kuifanya kwa sababu ni kitu kinachonigusa mimi mwenyewe. Nimefanya 'concerts' za 'praise and worship' mbalimbali ambazo ziliwakutanisha vijana wa mashuleni na vyuoni, na katika hizo 'concerts' wengi walimpokea Yesu. haitaishia hapa, nitaendelea nayo hii huduma na 'partners' wangu ambao wengi wao wameenda masomoni vyuo vingine."
Kwa kweli, utakubaliana na mimi kwamba tunahitaji watu wengi zaidi wenye moyo wa kumtumikia Mungu, wasio wavivu kujua Mungu anataka wafanye nini, na wanapopata kufahamu, wanachukua hatua na kuhakikisha kitu kimetokea si kwa kujifurahisha bali kwa kumpa Mungu utukufu!
Mungu ana watu wengi hivyo pamoja na wewe na mimi tutakaokuwepo kwenye tukio hilo, pia watakuwepo waimbaji mbali mbali kama The Living testimony, Paul Clement wa Glorious Celebration, kwaya za Casfeta na Uscf, Gadi Visima, Edward Mnyema Oliver Julius, Titho Buzuka na wengine wengi.
Titho Buzuka |
Paul Clement |
Ni uzinduzi unaoambatana na sifa na ibada kwa Mungu!Njoo umsifu Mungu, wekeza kwa BWANA! Hii si ya kukosa...
No comments:
Post a Comment