Sunday, February 17, 2013

NI KWANINI WANAFUNZI WANAKOSA NAFASI ZA KUFANYA FIELD?

HELLO WATANZANIA.HABARI ZENU!
NI UTARATIBU WA KAWAIDA KWA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU KUPATA MUDA WA KUFANYA MAZOEZI KATIKA OFISI MBALIMBALI ZA SERIKALI NA BINAFSI KILA BAADA YA MUDA FULANI WA MASOMO YAO,ILI KUPATA NAFASI YA KUYAFANYIA MAZOEZI YALE WALIOJIFUNZA KWA VITENDO!!

KUNA BAADHI YA KOZI AMBAZO WANAFUNZI NI LAZIMA WAFANYE ZOEZI TU KWA MKONO WA SERIKALI KWA KUWA NI "MUST" NA NI JUKUMU LA SRRIKALI YENYEWE, KWA MFANO KOZI ZA UALIMU,AFYA NA KILIMO NA KUZITAJA CHACHE!

LAKINI KUNA KOZI ZINGINE AMBAZO JUKUMU LA KUPATA NAFASI YA KUFANYA
MAOZOEZI NI KAZI YA CHUO AU TAASISI HUSIKA ANAYOSOMA AU MWANAFUNZI MWENYEWE!

NA KIMSINGI MAZOEZI HAYA NI AFYA YA AKILI YA MWANAFUNZI,MAANA HAPO NDIPO MWANAFUNZI ANAPOBADILI MTAZAMO WA NADHARIA KUJA KWA VITENDO,LAKINI PIA KUANZA KUJENGA MTANDAO MPYA NJE YA WANAFUNZI KULE CHUONI KWAKE!

NA KWA WALE WANAOPATA MIKOPO,HUPEWA FUNGU KWA AJILI YA MAZOEZI,HIVYO SIO KAZI YA OFISI INAYOMPOKEA KUMLIPA WALA KUMHUDUMIA ZAIDI YA KUMJENGEA MAZINGIRA TAKAYOFANYA KAZI KWA UTULIVU!

SASA NASHINDWA KUSHANGAA KUONA WATU WANAKOSAJE NAFASI ZA KUFANYA MAZOEZI HUKO MAOFISINI? TENA KUNA BAADHI YA MAOFISA UTUMISHI HUTAKA WAPEWE FEDHA(RUSHWA/TAKRIMA) ILI WARUHUSU WANAFUNZI WA VYUO KUFANYA MAZOEZI KATIKA OFISI ZAO,NA WENGINE HUTAKA MPAKA RUSHWA YA NGONO,WHY?

HIVI IKIWA UNAPATA MTU WA KUKUSAIDIA KAZI OFISINI KWAKO UNA HAJA GANI YA KUWEKA KAUZIBE? YAMKINI HUJAELEWA FAIDA YAKE LABDA!

ANGALIZO;
NA KWA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU NAPENDA KUTOA USHAURI KWENU KUWA,SIO LAZIMA UFANYE MAZOEZI MJINI AU KWENYE MAJIJI,UNAWEZA HATA UKAENDA MKOANI KWAKO NA WILAYANI KWAKO,MAANA KWA KUFANYA HIVYO,UTAKUWA SIO TU UNAFANYA MAZOEZI,BALI UTAKUWA UNATOA MCHANGO KWA MAENDELEO YA MJI WA KWENU!!

NI MUHIMU SERIKALI KUWAONYA NA KUWAELIMISHA WAFANYAKAZI WAKE,HUSUSANI MAOFISA WASIMAMIZI WA RASILIMALI WATU KUWA NI AFYA KUWALEA WANAFIUNZI MAANA HAO NDIO WATAALAMU WA SERIKALI WAJAO!!!

No comments:

Post a Comment