Saturday, December 1, 2012

ZAMU YA...... TITHO BUZUKA....!!!

KUTANA NA TITHO BUZUKA....!!!

Ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu katika chuo kikuu cha Dododoma - Informatics and Virtual Education anayechukua masomo ya "Computer and Information Security (CIS)" . 
Kwa wale wanaojua UDOM kwa kweli watakubaliana nami kwa jinsi ambavyo tumebarikiwa kuwa na waimbaji wengi wa nyimbo za Injili. Wengi wamezindua na sasa mbele yetu tunatarajia uzinduzi wa album ya Titho ambayo kwa kweli ni ya kipekee na nitakupa sababu mbili katika hili

kwanza ni ya nyimbo za kumsifu na kumuabudu Mungu ambazo zitakusogeza kwenye uwepo wa Mungu.

Pili zimeimbwa kwa ustadi ukizingatia kwamba Titho ni kijana mpole, mnyenyekevu na mwenye kumuheshimu Mungu lakini pia ana kipaji na karama katika eneo hilo.

Lakini katika hayo yote, nilimtafuta Titho mwenyewe nipate kujua walau mambo baadhi kuhusu album na siku yenyewe ya uzinduzi na wewe pia upate kujua kutoka kwake...

Aliniambia kwamba, ukiacha masomo anayosoma hapa, yeye ni muajiriwa katika shule ya sekondari Mugumu iliyopo Serengeti Musoma. Na pia ni mwanzilishi wa huduma ya "Healing Praise Ministry (HPM)". 

Akizungumzia kuhusu uzinduzi, alisema kuwa itakuwa siku ya Jumaamosi tarehe 8 mwezi wa 12 UDOM - Social Science katika ukumbi wa Taji Cafeteria  kuanzia saa kumi na moja jioni hadi saa sita usiku.

Bila kusahau kitu muhimu, jina la album!!

Alisema kuwa album inaitwa "NIGUSE" ambayo ina jumla ya nyimbo tisa. 

Haya sasa, nilitamani kujua nini kilichomsukuma kutengeneza album hiyo maana ni wengi wanaimba na kila mtu ana sababu zake za kufanya hivyo. Nini hasa sababu kwa upande wake, Titho alikuwa na haya ya kusema.

"Lengo hasa ni kumsifu na kumuabudu Mungu, dhima kubwa ya album ni kumuabudu Mungu, na haimaanishi ni nyimbo za taratibu tu."

Kuna jambo pia la kuhusiana na HPM. Nilitamani kujua zaidi kuhusu hilo.

Alisema kuwa, HPM ni huduma inayojihusisha hasa na kusifu, kuabudu na maombezi. Na pia wanajihusisha na mambo mengine kama "shooting, cover designing, doubling" na mengine mengi.

Nini hasa kilikusukuma kuanzisha HPM? Lilikuwa swali langu lingine na Titho alikuwa na haya ya kusema

"Nilikuja kugundua kwamba maisha yangu yanakamilishwa kwenye kumsifu na kumuabudu Mungu na ndio lengo hasa la kuanzisha HPM. Natamani hasa kumuinua Mungu na kuona watu wakiponywa, wakifunguliwa na kuwekwa huru. "


Turudi kwenye uzinduzi, nani pia wanatarajiwa kuwepo kuhudumu siku hiyo?

Aliniambia kuwa wapo waimbaji wengi kama
Joshua Ndaki
Jane Silomba
Gift Kalinga
Victor John
The Living Testimony
Casfeta Social Science Choir
Casfeta Education Choir
Casfeta UDOM Choir
Joshua Ndaki
Visima Gadi
Victor John
na wengine wengi



Kabla ya kumaliza mazungumzo yetu, nilitaka kusikia nini Titho anataka kuwaambia watu kuhusu uzinduzi wa album yake hiyo tarehe nane.....


"Watu wategemee uzinduzi wa album utakao ambatana na kusifu na kuabudu. Tuje tumuabudu Mungu!!!"
  

HII SI YA KUKOSA.... Jumaamosi tarehe nane Disemba pale Social Science UDOM!!!

1 comment:

  1. UDOM are blessed with powerfull singers! I can imagine what will happen there, there will be another downfall of satanic spirits. God bless you all.

    ReplyDelete