Thursday, April 25, 2013

CHUO CHA UHASIBU ARUSHA CHAFUNGWA KWA MUDA USIOJULIKANA!!!

 Chuo cha uhasibu arusha kimefungwa leo saa 12 jioni kutokana na kutoelewana kwa wanafunzi wa chuo hicho na mkuu wa mkoa Arusha.
jambo hili limetokea baada ya wanafunzi wa chuoni hapa kutaka kuandamana kwenda kwa mkuu wa mkoa kudai madai ya usalama wao kua mdogo kutokana na mauaji yaliyofanywa kwa mwanafunzi mwenzao HENRY KOGA kuchomwa kisu cha shingo na watu wasiojulikana na kumpola LAPTOP na mali zake nyingine.
kitendo hicho kiliwakumbusha machungu wanafunzi wa uhasibu kutokana kupita kipindi kifupi kupita tangu aliyekuwa mwanafunzi wa chuo hicho OCTAVIAN BUKAJUMBE kuchomwa kisu na kuuawa mazingira ya chuo hicho hata miezi miwili haijapita.
Kabla fujo na mabomu ya machozi kuanza kurushwa kila mahali wanafunzi walikutana chuoni eneo linaloitwa FREEDOM SQUARE wakipanga namna ya kuandamana kwenda kwa mkuu wa mkoa. RPC alifika pamoja na UONGOZI wa CHUO wakijaribu kuwazuia wanafunzi wasiandamane.
wanafunzi walionyesha kutowasikiliza wakimtaka MKUU WA CHUO ambaye alitafutwa bila mafanikio. kelele za wanafunzi zilipungua pale Mbunge wa jimbo la Arusha Godbless LEMA kufika chuoni hapa mnamo mida ya saa 4 asubuhi na kuwatuliza kwa kumpigia simu mkuu wa mkoa wa arusha kufika chuoni na kusikiliza madai ya wanafunzi hao. hasira za wanafunzi zilipanda baada ya mkuu wa mkoa kufika na kusema "hawezi kuongea na watu wasio na nidhamu" pia hawezi kuongea bila kipaza sauti akisahau kuwa wanafunzi hao wanauchungu na hasira za mwenzao kuuawa kinyama.
Mabomu yalianza kupigwa baada ya mkuu wa mkoa huyo kuonyesha kutojali kile wanafunzi wanachotaka. ndipo walipoanza kuzomea na kurusha chupa kwa mkuu wa mkoa na askari kuanza kupiga mabomu ya machozi...
Baadhi ya maafa yaliyotokea ni baadhi ya wanafunzi kuzimia na wengine kujeruhiwa na kuibiwa mali zao wengine wamekamatwa..wanafunzi waliobaki wametakiwa kurudi nyumbani kwao mikoa mbalimbali ndani ya Tanzania kwa muda usiojulikana.
Matukio ya uporaji na kujeruhiwa limekuwa tatizo sugu kwa wanafunzi wa uhasibu zaidi kwa wanafunzi wa kiume wasiokuwa na MABWENI chuoni hapo hivyo kulazimika kupanga maeneo ya karibu na chuoni hapo. ambapo hupata matatizo hayo wanapokuwa wakirudi magetoni mwao na wakati mwengine wamekuwa wakivamiwa huko huko kutokana na kutokuwa na usalama wowote.
Kimekuwa ni kilio jwa wanafunzi hao waweze kujengewa BWENI la wavulana mahali hapo bila kupata majibu yeyote.
Historia ya Marehemu
Jina: HENRY KOGA
Mwenyeji: IRINGA
Alikuwa anasoma: SHAHA YA FEDHA NA BENKI (mwaka 2)
Aliuwa: KWA KUCHOMWA KISU NA VIBAKA
Muda: KATI YA SAA 4 NA SAA 5 USIKU
Mahali: ESAMI Nje kidogo na geti la kuingilia CHUONI UHASIBU

No comments:

Post a Comment